Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waroma 4:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 tena awe baba ya kutahiriwa, kwa wale ambao si waliotahiriwa tu, bali pia wanazifuata nyayo za imani yake baba yetu Abrahamu aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Vilevile yeye ni baba wa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwa wametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njia ileile ya imani baba yetu Abrahamu aliyofuata kabla ya kutahiriwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Vilevile yeye ni baba wa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwa wametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njia ileile ya imani baba yetu Abrahamu aliyofuata kabla ya kutahiriwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Vilevile yeye ni baba wa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwa wametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njia ileile ya imani baba yetu Abrahamu aliyofuata kabla ya kutahiriwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Vivyo hivyo awe baba wa wale waliotahiriwa ambao si kwamba wametahiriwa tu, bali pia wanafuata mfano wa imani ambayo baba yetu Ibrahimu alikuwa nayo kabla ya kutahiriwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Vivyo hivyo awe baba wa wale waliotahiriwa ambao si kwamba wametahiriwa tu, bali pia wanafuata mfano wa imani ambayo baba yetu Ibrahimu alikuwa nayo kabla ya kutahiriwa.

Tazama sura Nakili

Waroma 4:12
14 Marejeleo ya Msalaba  

Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza.

Wakuu wa watu wamekusanyika, Kama watu wa Mungu wa Abrahamu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.

Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki.

Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake, Shika njia uzifuate nyayo za kondoo, Na kuwalisha wana-mbuzi wako Karibu na hema za wachungaji.

Mwanadamu, watu wale wakaao mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli husema ya kwamba, Abrahamu alikuwa mmoja, akairithi nchi hii; lakini sisi tu watu wengi; tumepewa nchi hii iwe urithi wetu.

wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.

Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, mhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;

Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Abrahamu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani.

Nilimwonya Tito, nikamtuma ndugu yule pamoja naye. Je! Tito aliwatoza kitu? Je! Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?

Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo