Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waroma 11:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimebaki peke yangu, nao wananitafuta roho yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 “Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 “Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 “Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Alisema, “Mwenyezi Mungu, wamewaua manabii wako na kuzibomoa madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Alisema, “Bwana Mungu, wamewaua manabii wako na kuzibomoa madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua?”

Tazama sura Nakili




Waroma 11:3
6 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Bwana wangu hakuambiwa nilivyofanya hapo Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA? Jinsi nilivyowaficha manabii wa BWANA, watu mia moja, hamsini hamsini katika pango, nikawalisha chakula na kuwapa maji?


kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia moja, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).


Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.


Nimewapiga watoto wako bure; hawakukubali kurudiwa; upanga wenu wenyewe umewala manabii wako, kama simba aharibuye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo