Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 9:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 na mafuta ya ng'ombe; na ya kondoo, mkia wake wa mafuta, na hayo yafunikayo matumbo, na figo zake, na kitambi cha ini;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mafuta ya fahali huyo na kondoo dume, mkia wa kondoo, mafuta yaliyofunika matumbo, figo na sehemu bora ya ini

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mafuta ya fahali huyo na kondoo dume, mkia wa kondoo, mafuta yaliyofunika matumbo, figo na sehemu bora ya ini

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mafuta ya fahali huyo na kondoo dume, mkia wa kondoo, mafuta yaliyofunika matumbo, figo na sehemu bora ya ini

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Lakini sehemu zile za mafuta ya yule maksai na ya yule kondoo dume, yaani mafuta ya mkia, yaliyofunika tumbo, ya figo na kipande kirefu cha ini,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Lakini sehemu zile za mafuta ya yule maksai na kondoo dume, yaani mafuta ya mkia, mafuta yaliyofunika tumbo, ya figo na yaliyofunika ini,

Tazama sura Nakili




Walawi 9:19
7 Marejeleo ya Msalaba  

Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani.


Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.


Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.


Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa BWANA, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,


lakini mafuta, na figo, na kitambi kilichotoka katika ini ya hiyo sadaka ya dhambi, akaviteketeza juu ya madhabahu, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


nao wakayaweka hayo mafuta juu ya vidari, naye akayateketeza mafuta juu ya madhabahu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo