Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 8:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Basi Musa akafanya kama alivyoambiwa na BWANA; na huo mkutano ulikutanishwa mlangoni pa hema ya kukutania.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akaikusanya jumuiya yote mbele ya mlango wa hema la mkutano.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akaikusanya jumuiya yote mbele ya mlango wa hema la mkutano.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akaikusanya jumuiya yote mbele ya mlango wa hema la mkutano.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Musa akafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza, na watu wakakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Musa akafanya kama bwana alivyomwagiza, na mkutano ukakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

Tazama sura Nakili




Walawi 8:4
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na zile nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyatengeneza hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Nao wakakikaza kile kifuko kwa pete zake kwenye naivera kwa ukanda wa rangi ya samawati, ili kikae pale juu ya mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, na ya kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.


njuga na komamanga, njuga na komamanga katika pindo za joho kuizunguka pande zote, ili kutumika kwa hiyo; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.


na huo mshipi wa nguo nzuri ya kitani iliyosokotwa, na rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, kazi ya fundi mwenye kutia taraza; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Na huo mshipi wa kazi ya werevu, uliokuwa juu yake ili kuifunga mahali pake; ulikuwa wa kitu kimoja, na wa kazi moja na naivera ya dhahabu, na rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Naye akavitia katika vile vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Kisha Musa akawaleta wana wa Haruni, na kuwavika kanzu, na kuwafunga mishipi, na kuwavika vilemba; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Lakini huyo ng'ombe mwenyewe, na ngozi yake, na nyama yake, na mavi yake, akaviteketeza nje ya kambi; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Kisha Musa akakitwaa kile kidari, akakitikisa huku na huko, kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; ni sehemu ya Musa katika huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


kisha ukutanishe mkutano wote hapo mlangoni pa hema ya kukutania.


Nanyi mtakaa mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba mchana na usiku, na kuulinda ulinzi wa BWANA ili kwamba msife; kwani ndivyo nilivyoagizwa.


Musa akawaambia mkutano, Neno aliloliagiza BWANA kwamba lifanywe, ni hili.


Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande cha dhahabu, hilo taji takatifu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Kwa maana mimi nilipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,


Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko;


Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo