Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Walawi 8:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya upande wa kulia, na katika vidole vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kulia; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Wanawe Aroni nao wakaja, naye Mose akawapaka kiasi cha damu kwenye ncha za masikio yao ya kulia, vidole gumba vya mikono yao ya kulia na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu nyingine akainyunyizia madhabahu pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Wanawe Aroni nao wakaja, naye Mose akawapaka kiasi cha damu kwenye ncha za masikio yao ya kulia, vidole gumba vya mikono yao ya kulia na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu nyingine akainyunyizia madhabahu pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Wanawe Aroni nao wakaja, naye Mose akawapaka kiasi cha damu kwenye ncha za masikio yao ya kulia, vidole gumba vya mikono yao ya kulia na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu nyingine akainyunyizia madhabahu pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Pia Musa akawaleta hao wana wa Haruni mbele, akaipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono yao ya kuume, na juu ya vidole vikubwa vya miguu yao ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Walawi 8:24
4 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Haruni la upande wa kulia, na katika ncha za masikio ya kulia ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kulia, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kandokando.

kisha huyo kuhani atatwaa baadhi ya hiyo damu ya sadaka ya hatia, naye kuhani ataitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;

Kisha akayatwaa hayo mafuta, na mkia wenye mafuta, na mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo, na kitambi cha ini, na figo mbili, na mafuta yake, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo