Walawi 6:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC
25 Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za BWANA; ni takatifu sana.
25 “Mwambie Aroni na wanawe kuwa ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa dhambi, mahali pale ambapo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa ndipo atakapochinjiwa mnyama wa sadaka ya kuondoa dhambi, mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka takatifu kabisa.

25 “Mwambie Haruni na wanawe: ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjiwa mbele za Mwenyezi Mungu mahali sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa; ni takatifu sana.
25 “Mwambie Haruni na wanawe: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjiwa mbele za bwana mahali sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, ni takatifu sana.
Kisha akaniambia, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao BWANA, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana, na sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia; kwa maana mahali hapo ni patakatifu.
Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za BWANA; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.
Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.
Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kandokando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania
Hautaokwa kwa chachu. Nimewapa kuwa sehemu yao katika matoleo yangu yasongezwayo kwa njia ya moto; ni kitu kitakatifu sana, kama hiyo sadaka ya dhambi, na kama hiyo sadaka ya hatia.
Kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo, na sadaka ya hatia ni vivyo hivyo; sheria yake ni moja; huyo kuhani afanyaye upatanisho kwayo, ndiye atakayekuwa nayo.