Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 6:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Na huyo kuhani aliyetiwa mafuta badala yake katika hao wanawe ataisongeza; itateketezwa kabisa kwa BWANA kwa amri ya milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Kuhani aliye mzawa wa Aroni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Kuhani aliye mzawa wa Aroni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Kuhani aliye mzawa wa Aroni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyepakwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la milele la Mwenyezi Mungu, nalo litateketezwa kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyetiwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la kawaida la bwana, nalo litateketezwa kabisa.

Tazama sura Nakili




Walawi 6:22
13 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;


Hujilisha dhambi ya watu wangu, hujifurahisha moyo kwa uovu wao.


Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.


kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.


kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.


Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu.


Kisha atayavua mavazi yake, na kuvaa mavazi mengine, kisha atayachukua yale majivu kwenda nayo nje ya kambi hata mahali safi.


Utaandaliwa kikaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowama utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Tena kila sadaka ya unga ya kuhani itateketezwa kabisa; isiliwe.


Kisha akayaosha matumbo na miguu yake kwa maji; na Musa akamteketeza huyo kondoo wote juu ya madhabahu; ilikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza; ilikuwa ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


(Wana wa Israeli wakasafiri kutoka visima vya Bene-yaakani kwenda Mosera; Haruni akafa huko, akazikwa huko; na Eleazari mwanawe akahudumu kama kuhani badala yake.


Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu walizuiliwa na mauti wasikae;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo