Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 6:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Kila mwanamume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya BWANA yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu yeyote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Wazawa wa kiume wa Aroni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa daima kwa ajili yao kutoka sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mtakatifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Wazawa wa kiume wa Aroni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa daima kwa ajili yao kutoka sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mtakatifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Wazawa wa kiume wa Aroni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa daima kwa ajili yao kutoka sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mtakatifu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kila mwanaume mzao wa Haruni aweza kuila. Ni fungu lake milele la sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto kwa vizazi vijavyo. Chochote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kila mwanaume mzao wa Haruni aweza kuila. Ni fungu lake la kawaida la sadaka zilizotolewa kwa bwana kwa moto kwa vizazi vijavyo. Chochote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”

Tazama sura Nakili




Walawi 6:18
19 Marejeleo ya Msalaba  

Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.


Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.


kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.


kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.


Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa.


Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu.


BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Kila kitu kitakachoigusa nyama ya sadaka hiyo kitakuwa kitakatifu; tena itakapomwagika damu yake yeyote katika nguo yoyote, utaifua nguo hiyo iliyomwagiwa, katika mahali patakatifu.


Kila mwanamume miongoni mwa makuhani atakula katika hiyo; ni takatifu sana.


Kila mwanamume miongoni mwa makuhani atakula katika sadaka hiyo; italiwa katika mahali patakatifu; ni takatifu sana.


Utakula vitu hivyo kuwa ni vitu vitakatifu sana; kila mwanamume atakula vitu hivyo; vitakuwa vitakatifu kwako wewe.


Kisha BWANA akamwambia Haruni, Tazama, nimekupa wewe ulinzi wa sadaka zangu za kuinuliwa, maana, vitu vyote vya hao wana wa Israeli vilivyowekwa wakfu; nimekupa wewe na wanao vitu hivyo kwa ajili ya kule kutiwa mafuta kwenu, kuwa haki yenu milele.


Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiayo madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?


kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.


Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo