Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 5:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Ni sadaka ya hatia; hakika yake ni mwenye hatia mbele za BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Hiyo ni sadaka ya hatia; yeye ana hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Hiyo ni sadaka ya hatia; yeye ana hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Hiyo ni sadaka ya hatia; yeye ana hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi ya Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi ya bwana.”

Tazama sura Nakili




Walawi 5:19
10 Marejeleo ya Msalaba  

Hata Shekania, mwana wa Yehieli, mmoja wa wazawa wa Elamu, akajibu, akamwambia Ezra, Sisi tumemkosea Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini bado kuna tumaini kwa Israeli katika jambo hili.


Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.


Na katika ukumbi wa lango palikuwa na meza mbili upande huu, na meza mbili upande huu, ili kuichinja sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia.


Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia pia, naye atachukua uovu wake.


Naye ataleta kondoo dume wa kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, amsongeze kwa huyo kuhani; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya jambo hilo alilolikosa pasipo kukusudia, asilijue, naye atasamehewa.


Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.


BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.


Nao wakawafikia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo