Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 5:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia pia, naye atachukua uovu wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 “Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 “Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 “Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 “Kama mtu akifanya dhambi, na kutenda yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 “Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za bwana, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.

Tazama sura Nakili




Walawi 5:17
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.


Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi bila kukusudia, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;


Mtawala atakapofanya dhambi, na kutenda pasipo kukusudia neno lolote kati ya hayo ambayo BWANA, Mungu wake, aliyazuilia yasifanywe, naye amepata hatia;


Na mtu yeyote kati ya watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, naye akapata hatia;


Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya BWANA; ndipo atakapomletea BWANA sadaka yake ya hatia, kondoo dume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia;


Naye ataleta kondoo dume wa kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, amsongeze kwa huyo kuhani; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya jambo hilo alilolikosa pasipo kukusudia, asilijue, naye atasamehewa.


Ni sadaka ya hatia; hakika yake ni mwenye hatia mbele za BWANA.


Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.


Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo