Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 4:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Na mtu yeyote kati ya watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, naye akapata hatia;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 “Kama mtu wa kawaida ametenda dhambi bila kukusudia, kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu na hivyo akawa na hatia,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 “Kama mtu wa kawaida ametenda dhambi bila kukusudia, kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu na hivyo akawa na hatia,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 “Kama mtu wa kawaida ametenda dhambi bila kukusudia, kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu na hivyo akawa na hatia,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 “ ‘Kama mtu katika jumuiya ametenda dhambi pasipo kukusudia, na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Mwenyezi Mungu, yeye ana hatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 “ ‘Kama mtu katika jumuiya ametenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya bwana, yeye ana hatia.

Tazama sura Nakili




Walawi 4:27
14 Marejeleo ya Msalaba  

Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.


Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini.


Tena itakuwa kazi ya mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji, katika sikukuu, na katika mwezi mpya, na katika sabato, katika sikukuu zote za nyumba ya Israeli zilizoamriwa; atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli.


Nawe utafanya vivyo hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi kwa ajili ya kila mtu akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia nyumba upatanisho.


Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi bila kukusudia, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;


Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu yeyote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lolote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lolote la maneno hayo;


Mtawala atakapofanya dhambi, na kutenda pasipo kukusudia neno lolote kati ya hayo ambayo BWANA, Mungu wake, aliyazuilia yasifanywe, naye amepata hatia;


Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia pia, naye atachukua uovu wake.


Kisha akaisongeza dhabihu ya watu, akamtwaa mbuzi wa sadaka ya dhambi aliyekuwa kwa hao watu, na kumchinja, na kumtoa kwa ajili ya dhambi kama yule wa kwanza.


Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi.


Tena mtakapokosa, msiyashike maagizo hayo yote BWANA aliyomwambia Musa,


Tena kama mtu mmoja akifanya dhambi pasipo kujua, ndipo atasongeza mbuzi mmoja wa kike wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya dhambi.


Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lolote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.


Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yoyote, ifanywayo na binadamu, kumwasi BWANA, na mtu huyo akawa na hatia;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo