Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 25:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Ikiwa nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 “Kama ndugu yako anakuwa maskini, akauza ardhi yake, basi, ndugu yake wa karibu mwenye jukumu la kuikomboa, ataikomboa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 “Kama ndugu yako anakuwa maskini, akauza ardhi yake, basi, ndugu yake wa karibu mwenye jukumu la kuikomboa, ataikomboa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 “Kama ndugu yako anakuwa maskini, akauza ardhi yake, basi, ndugu yake wa karibu mwenye jukumu la kuikomboa, ataikomboa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini na akauza baadhi ya mali yake, ndugu yake wa karibu atakuja na kukomboa kile ndugu yake alichokiuza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini na akauza baadhi ya mali yake, ndugu yake wa karibu atakuja na kukomboa kile ndugu yako alichokiuza.

Tazama sura Nakili




Walawi 25:25
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nanyi mtatoa ukombozi kwa ajili ya nchi, katika eneo lote la milki yenu.


Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa;


Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni;


Tena kama akiweka wakfu kwa BWANA shamba ambalo amelinunua, ambalo si shamba la milki yake;


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,


Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na BWANA, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwa waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa ukoo wetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.


Tena ni kweli kuwa mimi ni jamaa yako aliye karibu; lakini kuna mtu wa jamaa aliye karibu kuliko mimi.


Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani.


Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu.


Kisha akamwambia yule jamaa, Huyu Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi aliyokuwa nayo ndugu yetu, Elimeleki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo