Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 25:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kuwatangazia uhuru watu wote katika nchi; itakuwa ni mwaka wa jubilii kwenu; na kila mtu atairudia milki yake, na kila mtu atarejea kwa jamaa yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini. Kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini. Kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini. Kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni Yubile kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni yubile kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake.

Tazama sura Nakili




Walawi 25:10
30 Marejeleo ya Msalaba  

Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya BWANA, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.


Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; BWANA hufungua waliofungwa;


Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.


kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza, Jionesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho.


Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu, Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.


na wakuu wote, na watu wote, wakati, waliofanya agano hilo, ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake na mjakazi wake, mtu yeyote asiwatumikishe tena; wakatii, wakawaacha.


Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule mfalme Sedekia alipofanya agano na watu wote waliokuwa katika Yerusalemu, kuwatangazia habari za uhuru;


Bali akimpa mmoja wa watumishi wake baadhi ya urithi wake, itakuwa mali yake mpaka mwaka wa kuacha huru; ndipo itakapomrudia mkuu; lakini urithi wake, huo utakuwa wa wanawe.


Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni jubilii kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.


Mwaka huo wa jubilii mtairudia kila mtu milki yake.


ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake.


Tena kwamba hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, ndipo atatoka katika mwaka wa jubilii, yeye, pamoja na watoto wake.


Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,


Basi “Bwana” ndiye Roho; lakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.


Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa yuko utumwani pamoja na watoto wake.


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.


kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo