Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Walawi 23:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

36 Mtamsogezea BWANA sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamtolea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Kwa muda wa siku saba mtatoa sadaka anazopewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa. Mkutano huo ni mtakatifu. Siku hiyo msifanye kazi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Kwa muda wa siku saba mtatoa sadaka anazopewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa. Mkutano huo ni mtakatifu. Siku hiyo msifanye kazi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Kwa muda wa siku saba mtatoa sadaka anazopewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa. Mkutano huo ni mtakatifu. Siku hiyo msifanye kazi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Kwa siku saba toeni sadaka kwa Mwenyezi Mungu za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Kwa siku saba toeni sadaka kwa bwana za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na mtoe sadaka kwa bwana ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.

Tazama sura Nakili

Walawi 23:36
8 Marejeleo ya Msalaba  

Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hadi siku ya mwisho, akasoma katika kitabu cha Torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusanyiko la makini, kama ilivyoagizwa.

Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu;

Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yoyote ya utumishi.

Katika siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa BWANA, Mungu wako, usifanye kazi yoyote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo