Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Walawi 23:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA, pamoja na wale wana-kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa BWANA, wawe wa huyo kuhani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Kuhani atavipitisha mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu viwe sadaka ya kutoa kwa ishara pamoja na mkate wa mavuno ya kwanza na wale wanakondoo wawili. Vitu hivyo ni vitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu navyo vitakuwa kwa matumizi ya kuhani tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Kuhani atavipitisha mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu viwe sadaka ya kutoa kwa ishara pamoja na mkate wa mavuno ya kwanza na wale wanakondoo wawili. Vitu hivyo ni vitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu navyo vitakuwa kwa matumizi ya kuhani tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Kuhani atavipitisha mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu viwe sadaka ya kutoa kwa ishara pamoja na mkate wa mavuno ya kwanza na wale wanakondoo wawili. Vitu hivyo ni vitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu navyo vitakuwa kwa matumizi ya kuhani tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kuhani atawainua hao wana-kondoo wawili mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa, pamoja na mkate wa malimbuko. Ni sadaka takatifu kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kuhani atawainua hao wana-kondoo wawili mbele za bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa, pamoja na mkate wa malimbuko. Ni sadaka takatifu kwa bwana kwa ajili ya kuhani.

Tazama sura Nakili

Walawi 23:20
12 Marejeleo ya Msalaba  

nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisatikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.

Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA.

Nanyi mtasongeza mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili wa kiume wa mwaka wa kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani.

Nanyi mtatangaza suku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yoyote ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu.

Kisha Musa akakitwaa kile kidari, akakitikisa huku na huko, kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; ni sehemu ya Musa katika huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.

Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?

Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.

Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo wako, umpe.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo