Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 23:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Pamoja na sadaka hiyo, mtatoa sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni lita moja ya divai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Pamoja na sadaka hiyo, mtatoa sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni lita moja ya divai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Pamoja na sadaka hiyo, mtatoa sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni lita moja ya divai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 pamoja na sadaka yake ya nafaka ya sehemu mbili za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto; hii itakuwa sadaka iliyo harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka yake ya kinywaji ya robo ya hini ya divai.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 pamoja na sadaka yake ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa bwana kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka yake ya kinywaji ya robo ya hini ya divai.

Tazama sura Nakili




Walawi 23:13
15 Marejeleo ya Msalaba  

na kida shekeli mia tano, kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu, na mafuta ya zeituni kiasi cha vibaba vitano;


Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hamtamimina juu yake sadaka ya kinywaji.


Nawe utakunywa maji kwa kuyapima, sehemu ya sita ya hini; utayanywa kwa wakati wake.


Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe, na efa moja kwa kondoo dume, na hini moja ya mafuta kwa efa moja;


Nawe utaitoa sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa BWANA daima, kwa amri ya milele.


Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njooni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.


Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA; Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.


Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?


Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili wa kiume wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.


Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume asiye na dosari wa mwaka wa kwanza, awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.


Matoleo ya Haruni na wanawe watakayomtolea BWANA, katika siku atakayotiwa mafuta, ni haya; sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga daima, nusu yake asubuhi, na nusu yake jioni.


hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo