Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 22:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Na mtu yeyote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda, katika ng'ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema chochote ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mtu yeyote anapomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya amani ili kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari kutoka katika kundi lake la mifugo, ili akubaliwe ni lazima awe ni mnyama mkamilifu; mnyama huyo asiwe na dosari yoyote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mtu yeyote anapomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya amani ili kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari kutoka katika kundi lake la mifugo, ili akubaliwe ni lazima awe ni mnyama mkamilifu; mnyama huyo asiwe na dosari yoyote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mtu yeyote anapomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya amani ili kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari kutoka katika kundi lake la mifugo, ili akubaliwe ni lazima awe ni mnyama mkamilifu; mnyama huyo asiwe na dosari yoyote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Mtu yeyote aletapo sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu kutoka kundi la ng’ombe au la mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Mtu yeyote aletapo sadaka ya amani kwa bwana kutoka kundi la ng’ombe au mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike.

Tazama sura Nakili




Walawi 22:21
13 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, wanaume kwa wanawake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.


Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;


Kipofu, au aliyevunjika mahali, au kiwete au aliye na vidonda, au aliye na upele, au aliye na upele, hamtamtolea BWANA wanyama hao, wala msiwasongeze kwa BWANA kwa njia ya moto juu ya madhabahu.


Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, dume au jike, atamtoa huyo asiye na dosari mbele ya BWANA.


Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; dume au jike, atamtoa huyo aliye mkamilifu.


nanyi mwataka kumsogezea BWANA sadaka kwa moto, kwamba ni sadaka ya kuteketezwa, au dhabihu ya kuchinjwa, ili kuondoa nadhiri, au iwe sadaka ya hiari, au katika sikukuu zenu zilizoamriwa, ili kumfanyia BWANA harufu ipendezayo, katika ng'ombe, au katika kondoo;


Tena hapo utakapomwandaa ng'ombe dume kwa sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa kuondoa nadhiri, au kwa sadaka za amani kwa BWANA;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo