Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 22:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Lakini mnyama yeyote aliye na kilema msimtoe; kwa kuwa hatakubaliwa kwa ajili yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Ni marufuku kutoa chochote kilicho na dosari kwani hakitakubaliwa kwa faida yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Ni marufuku kutoa chochote kilicho na dosari kwani hakitakubaliwa kwa faida yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Ni marufuku kutoa chochote kilicho na dosari kwani hakitakubaliwa kwa faida yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kamwe usitoe kitu chochote chenye dosari kwa sababu hakitakubaliwa kwa niaba yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kamwe usitoe kitu chochote chenye dosari kwa sababu hakitakubaliwa kwa niaba yako.

Tazama sura Nakili




Walawi 22:20
14 Marejeleo ya Msalaba  

Bwana MUNGU asema hivi; Mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utatwaa ng'ombe dume mchanga na mkamilifu; nawe utapatakasa mahali patakatifu.


Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.


Mnyama aliyeumia mapumbu yake, au kusetwa, au kuvunjwa, au kukatwa, msimtolee BWANA; wala msifanye hivi katika nchi yenu.


Wala msisongeze chakula cha Mungu wenu katika wanyama hao mmojawapo kitokacho mkononi mwa mgeni; kwa sababu uharibifu wao uko ndani yao, wana kilema ndani yao; hawatakubaliwa kwa ajili yenu.


Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, dume au jike, atamtoa huyo asiye na dosari mbele ya BWANA.


Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; dume au jike, atamtoa huyo aliye mkamilifu.


Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee mtawala wako; Je, Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi.


Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng'ombe jike mwekundu asiye na doa, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;


lakini mtamsogezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja; watakuwa wakamilifu kwenu;


Lakini akiwa na kilema, akichechea, au akiwa kipofu, au mwenye kilema kibaya chochote, usimsongezee BWANA, Mungu wako, sadaka.


Usimchinjie BWANA, Mungu wako, ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lolote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.


basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na dosari, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala waa, yaani, ya Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo