Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 19:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 “Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 “Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 “Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 “ ‘Ukiwa mbele ya mzee, simama ili kuonesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 “ ‘Uwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi bwana.

Tazama sura Nakili




Walawi 19:32
15 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.


Yusufu akawatoa katika magoti yake, naye akainama kifudifudi


Basi Bathsheba akaingia kwa mfalme Sulemani, aseme naye kwa ajili ya Adonia. Naye mfalme akainuka kwenda kumlaki, akamwinamia, akaketi katika kiti chake cha enzi; kisha akaagiza awekewe kiti cha enzi mamaye mfalme; naye akaketi mkono wake wa kulia.


ila yeye BWANA, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri kwa nguvu nyingi, na kwa mkono ulionyoshwa, yeye ndiye mtakayemcha, yeye ndiye mtakayemsujudia, yeye ndiye mtakayemtolea sadaka;


Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye.


Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema, Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana; Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonesha nionavyo.


Kichwa chenye mvi ni taji la utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki.


Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.


Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.


Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake; mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.


Wakuu hutundikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima.


Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.


Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.


Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na wanaume vijana kama ndugu;


Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo