Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 14:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Huyo ambaye ndani yake mna pigo la ukoma, ambaye hawezi kukipata hicho kipasacho kutakaswa kwake, sheria yake ni hiyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Huo ndio mwongozo kuhusu mtu mwenye ukoma asiyeweza kutoa sadaka za kumtakasa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Huo ndio mwongozo kuhusu mtu mwenye ukoma asiyeweza kutoa sadaka za kumtakasa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Huo ndio mwongozo kuhusu mtu mwenye ukoma asiyeweza kutoa sadaka za kumtakasa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Haya ndio masharti kwa mtu yeyote mwenye ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, na ambaye hana uwezo wa kutoa sadaka za kawaida kwa ajili ya kutakaswa kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Haya ndiyo masharti kwa mtu yeyote mwenye ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, na ambaye hana uwezo wa kutoa sadaka za kawaida kwa ajili ya kutakaswa kwake.

Tazama sura Nakili




Walawi 14:32
12 Marejeleo ya Msalaba  

Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Mtu atakapokuwa na uvimbe katika ngozi ya mwili wake, au upele, au kipaku king'aacho, nao ukawa ni ugonjwa wa ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa mmojawapo wa wanawe makuhani;


Na katika pigo la ukoma katika vazi la sufu, au la kitani, kama ni katika lililofumwa, au lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, sheria yake ni hiyo, kusema kwamba ni safi, au kusema kwamba ni najisi.


Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili wa kiume wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.


Hii ndiyo sheria ya mwenye ukoma, katika siku ya kutakaswa kwake; ataletwa kwa kuhani,


Lakini akiwa ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;


hata kadiri aliyoweza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya unga; na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa mbele za BWANA.


BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,


vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo