Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 13:50 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

50 na kuhani ataliangalia hilo pigo, naye atakiweka mahali kile kilicho na pigo muda wa siku saba;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

50 Kuhani atauangalia upele huo na kuliweka vazi hilo kando kwa muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

50 Kuhani atauangalia upele huo na kuliweka vazi hilo kando kwa muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

50 Kuhani atauangalia upele huo na kuliweka vazi hilo kando kwa muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

50 Kuhani atachunguza ukoma huo na kulitenga vazi hilo kwa siku saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

50 Kuhani atachunguza upele huo na kukitenga kifaa hicho kwa siku saba.

Tazama sura Nakili




Walawi 13:50
5 Marejeleo ya Msalaba  

Nao watawafundisha watu wangu tofauti iliyoko kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida, na kuwafundisha kupambanua kati ya yaliyo machafu na yaliyo safi.


Lakini ikiwa kipaku king'aacho katika ngozi ya mwili wake ni cheupe, na kuonekana si shimo la kuingia ndani kuliko ngozi wala nywele hazikugeuka kuwa nyeupe, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba huyo aliye na hilo pigo;


hilo pigo likiwa la rangi ya kijani au jekundu, katika vazi, au katika ngozi, au katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi; ni pigo la ukoma, nalo ataoneshwa kuhani;


kisha siku ya saba ataliangalia hilo pigo; kama pigo limeenea katika hilo lililofumwa, au katika hilo lililosokotwa, au katika ngozi, ijapokuwa hiyo ngozi ina matumizi yoyote; hilo pigo ni ukoma unaona; vazi hilo ni najisi.


ndipo kuhani atatoka katika nyumba hiyo mpaka mlangoni pa nyumba, na kuifunga hiyo nyumba muda wa siku saba;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo