Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Walawi 13:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 ndipo kuhani ataliangalia hilo pigo; ikiwa pigo limeingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na nywele zilizomo kuwa za rangi ya manjano na nyembamba, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi, maana ni kipwepwe, ni ukoma wa kichwa au wa kindevu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 kuhani atauangalia ugonjwa huo. Iwapo kuhani ataona kuwa kuna shimo na nywele ni manjano na nyembamba, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani huo ni upele na ni ukoma wa kichwa au wa kidevu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 kuhani atauangalia ugonjwa huo. Iwapo kuhani ataona kuwa kuna shimo na nywele ni manjano na nyembamba, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani huo ni upele na ni ukoma wa kichwa au wa kidevu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 kuhani atauangalia ugonjwa huo. Iwapo kuhani ataona kuwa kuna shimo na nywele ni manjano na nyembamba, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani huo ni upele na ni ukoma wa kichwa au wa kidevu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 kuhani atakichunguza kile kidonda, na kama ataona kuwa kimeingia ndani ya ngozi, na nywele zilizo juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 kuhani atakichunguza kile kidonda, na kama ataona kuwa kimeingia ndani, na nywele zilizoko juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi, kwani ni upele; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu.

Tazama sura Nakili

Walawi 13:30
5 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanamume au mwanamke atakapopatwa na maradhi kichani au kidevuni,

Tena kuhani akiliangalia lile pigo la kipwepwe, ikiwa kumeonekana si kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, wala hamna nywele nyeusi ndani yake, ndipo kuhani atamweka mahali huyo aliye na pigo la kipwepwe muda wa siku saba;

na siku ya saba kuhani ataliangalia hilo pigo; na ikiwa hicho kipwepwe hakikuenea, wala hamna nywele za rangi ya manjano ndani yake, na kwamba kipwepwe hakionekani kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe,

Hiyo ndiyo sheria ya pigo la ukoma ya kila aina, na ya kipwepwe;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo