Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Walawi 11:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

33 Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Ikiwa mzoga wake umeangukia chombo cha udongo, basi, chochote kilicho ndani ya chombo hicho ni najisi na lazima chombo hicho kivunjwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Ikiwa mzoga wake umeangukia chombo cha udongo, basi, chochote kilicho ndani ya chombo hicho ni najisi na lazima chombo hicho kivunjwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Ikiwa mzoga wake umeangukia chombo cha udongo, basi, chochote kilicho ndani ya chombo hicho ni najisi na lazima chombo hicho kivunjwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Ikiwa mmoja wa wanyama aliyekufa ataangukia ndani ya chungu, kila kilichomo katika chungu hicho kitakuwa najisi, nawe ni lazima uvunje chungu hicho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Ikiwa mmoja wa wanyama aliyekufa ataangukia ndani ya chungu, kila kilichomo katika chungu hicho kitakuwa najisi, nawe ni lazima uvunje chungu hicho.

Tazama sura Nakili




Walawi 11:33
11 Marejeleo ya Msalaba  

Juu ya madari yote ya nyumba za Moabu, na katika njia kuu zake, pana maombolezo, kila mahali; kwa maana nimevunja Moabu kama chombo kisichopendeza, asema BWANA.


Chakula chochote cha kuliwa kitakuwa najisi kikitiwa maji ya chombo hicho; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi.


Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande chochote cha mizoga yao kitakuwa najisi; iwe ni tanuri, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu.


Naye ataliteketeza vazi hilo, liwe ni la kufumwa au ni la kusokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu chochote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaona; vazi hilo litateketezwa;


Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hadi mahali palipo na uchafu.


Na chombo cha udongo ambacho amekigusa mwenye kisonono, kitavunjwavunjwa; na kila chombo cha mti kitaoshwa majini.


Utaandaliwa kikaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowama utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Lakini hicho chombo cha udongo ambacho hiyo nyama ilipikwa ndani yake kitavunjwa; na kama ikipikwa katika chombo cha shaba, kitasuguliwa, na kuoshwa kwa maji.


Na kila chombo kilicho wazi, kisichofungwa na kifuniko, ni najisi.


atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo