Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wakolosai 2:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 nanyi mmepewa uhai kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 nanyi mmepewa uhai kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 nanyi mmepewa uhai kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Al-Masihi, aliye mkuu juu ya kila nguvu na kila mamlaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Al-Masihi, ambaye ndiye mkuu juu ya kila enzi na kila mamlaka.

Tazama sura Nakili




Wakolosai 2:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.


Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.


Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.


ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;


na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.


akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuziaibisha hadharani, akiziongoza kwa ushindi wake wa shangwe.


Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.


naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


Naye yuko katika mkono wa kulia wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo