Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Wagalatia 6:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; huwataka nyinyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; huwataka nyinyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; huwataka nyinyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Hata wale waliotahiriwa wenyewe hawaitii sheria, lakini wanataka ninyi mtahiriwe ili wapate kujivuna kwa habari ya miili yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Hata wale waliotahiriwa wenyewe hawaitii sheria, lakini wanataka ninyi mtahiriwe ili wapate kujivuna kwa habari ya miili yenu.

Tazama sura Nakili

Wagalatia 6:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa Jehanamu mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.

Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

basi, yoyote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.

Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya.

Basi, mtu yeyote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu;

Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?

Kwa sababu wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili, mimi nami nitajisifu.

Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.

wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo