Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wagalatia 5:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Kwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kupitia kwa upendo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Kwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

Tazama sura Nakili




Wagalatia 5:6
22 Marejeleo ya Msalaba  

maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.


Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.


Kutahiriwa si kitu, na kutotahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.


Maana, upendo wa Kristo watuongoza; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote;


Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.


Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.


Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutotahiriwa, ila kiumbe kipya.


Amani na iwe kwa ndugu, na upendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.


tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;


Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.


Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na subira yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.


Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.


Kwa kuwa watu wote waliotoka walikuwa wamekwisha kutahiriwa; lakini watu wote waliozaliwa katika safari jangwani walipokwisha kutoka Misri, hao hawakutahiriwa.


Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo