Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wagalatia 5:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidi neno.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba mkikubali kutahiriwa, basi Al-Masihi hatakuwa na thamani kwenu hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Al-Masihi hatawafaidia chochote.

Tazama sura Nakili




Wagalatia 5:2
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wakashuka watu waliotoka Yudea wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamuwezi kuokoka.


Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza;


Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.


Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe.


Basi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu;


Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Kwa kufanya hivyo kikwazo cha msalaba kimeondolewa!


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, nilitaka kuja mara kwa mara, lakini Shetani akatuzuia.


Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakudai hata nafsi yako.


lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ndimi, Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia.


Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa Habari Njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo