Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wagalatia 5:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewasumbua atachukua hukumu yake, awaye yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba nyinyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni – awe nani au nani – hakika ataadhibiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba nyinyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni – awe nani au nani – hakika ataadhibiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba nyinyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni — awe nani au nani — hakika ataadhibiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Nina hakika katika Bwana Isa kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Nina hakika katika Bwana Isa kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani.

Tazama sura Nakili




Wagalatia 5:10
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza;


kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.


Nami nikiwa na tumaini hilo nilitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili;


naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.


tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.


Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.


Nami niliwaandikia neno lilo hilo, ili nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumaini ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.


Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi;


Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.


Nafurahi, kwa sababu katika kila neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu.


Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi kuwa ana bidii katika mambo mengi, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.


Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza Injili ya Kristo.


Bali kwa ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri; ambao waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani;


Lakini wale viongozi waliosifika kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyovyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao waliosifika hawakuniongezea kitu;


Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulubiwa?


Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha bure kwa ajili yenu.


Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa nia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku.


laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu.


Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!


Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli?


Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.


Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mungu atawafunulia hilo nalo.


Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza na kwamba mtaendelea kuyafanya.


Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.


Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo