Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wagalatia 3:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Nyinyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Nyinyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Nyinyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Al-Masihi, mmemvaa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Al-Masihi, mmemvaa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Wagalatia 3:27
20 Marejeleo ya Msalaba  

Nilijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.


Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.


Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;


Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatusihi sana.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.


Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;


Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.


ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;


wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wagiriki; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


na mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.


mkivaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu kulingana na mfano wake yeye aliyeuumba.


Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo