Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wagalatia 3:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Basi, hiyo sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo, ili kwa njia ya imani tufanywe waadilifu mbele yake Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Basi, hiyo sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo, ili kwa njia ya imani tufanywe waadilifu mbele yake Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Basi, hiyo sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo, ili kwa njia ya imani tufanywe waadilifu mbele yake Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Hivyo, Torati ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Al-Masihi, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Al-Masihi, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani.

Tazama sura Nakili




Wagalatia 3:24
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.


Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani;


Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu elfu kumi katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.


Lakini tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.


Maana mimi kwa njia ya sheria niliifia sheria ili nimwishie Mungu.


Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.


mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo