Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wagalatia 3:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Kabla ya kujaliwa imani, sheria ilitufanya wafungwa, tukingojea imani hiyo ifunuliwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Kabla ya kujaliwa imani, sheria ilitufanya wafungwa, tukingojea imani hiyo ifunuliwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Kabla ya kujaliwa imani, sheria ilitufanya wafungwa, tukingojea imani hiyo ifunuliwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya Torati, tumefungwa hadi ile imani ifunuliwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe.

Tazama sura Nakili




Wagalatia 3:23
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.


Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.


Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;


Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hadi aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.


Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria?


Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.


Hawa wote wakafa katika imani, walikuwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.


tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo