Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wagalatia 3:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa njia ya ahadi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Maana, kama zawadi ya Mungu inategemea sheria, basi, haiwezi kutegemea tena ahadi ya Mungu. Kumbe, lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa sababu aliahidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Maana, kama zawadi ya Mungu inategemea sheria, basi, haiwezi kutegemea tena ahadi ya Mungu. Kumbe, lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa sababu aliahidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Maana, kama zawadi ya Mungu inategemea sheria, basi, haiwezi kutegemea tena ahadi ya Mungu. Kumbe, lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa sababu aliahidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa maana kama urithi hupatikana kwa Torati, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Ibrahimu urithi kupitia kwa ahadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Ibrahimu urithi kwa njia ya ahadi.

Tazama sura Nakili




Wagalatia 3:18
14 Marejeleo ya Msalaba  

Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Abrahamu, mtumishi wake.


na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.


Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure.


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye.


Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo.


Basi ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazawa, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.


Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.


Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi kulingana na ahadi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo