Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 9:49 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

49 Basi watu hao wote wakakata kila mtu tawi lake, wakamfuata Abimeleki, wakayaweka hayo matawi pale ngomeni, na kuiteketeza moto hiyo ngome juu yao; ndipo watu wote wa huo mnara wa Shekemu wakafa, watu wapatao elfu moja, wanaume kwa wanawake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

49 Kila mmoja akakata tawi kama lile la Abimeleki. Wakachukua matawi yao na kuyaegemeza kwenye kuta za ngome, wakayatia moto na kuichoma ngome; watu wote wanaume na wanawake wapatao 1,000 waliokuwa katika mnara wa Shekemu wakafa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

49 Kila mmoja akakata tawi kama lile la Abimeleki. Wakachukua matawi yao na kuyaegemeza kwenye kuta za ngome, wakayatia moto na kuichoma ngome; watu wote wanaume na wanawake wapatao 1,000 waliokuwa katika mnara wa Shekemu wakafa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

49 Kila mmoja akakata tawi kama lile la Abimeleki. Wakachukua matawi yao na kuyaegemeza kwenye kuta za ngome, wakayatia moto na kuichoma ngome; watu wote wanaume na wanawake wapatao 1,000 waliokuwa katika mnara wa Shekemu wakafa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

49 Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome, na kuitia moto ili kuwachoma watu wote waliokuwa ndani. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, yamkini wanaume na wanawake elfu moja, pia wakafa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

49 Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome na kuitia moto ili kuwachoma wale watu wote waliokuwa ndani yake. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, karibia watu 1,000 waume kwa wake, pia wakafa.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 9:49
6 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.

Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.

Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Ikiwa kwa kweli mnanitia mafuta niwe mfalme juu yenu, basi njoni mkakae chini ya kivuli changu; la sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.

lakini ikiwa basi moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki.

Basi Abimeleki akakwea kwenda katika kilima cha Salmoni, yeye na wote waliokuwa pamoja naye; naye Abimeleki akashika shoka mkononi mwake, akakata tawi moja katika miti, akalishika na kujitwika begani mwake; akawaambia hao watu waliokuwa pamoja naye, “Haya, kile mlichoona nikifanya, nanyi fanyeni vivyo hivyo haraka”.

Ndipo Abimeleki alipokwenda Thebesi, akauzingira na kuutwaa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo