Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 9:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Kisha Mungu akatuma roho mbaya kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu; nao watu wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa udanganyifu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Kisha Mungu akaleta roho ya uadui kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu, nao wakamwasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Kisha Mungu akaleta roho ya uadui kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu, nao wakamwasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Kisha Mungu akaleta roho ya uadui kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu, nao wakamwasi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Mungu akaruhusu roho mbaya kati ya Abimeleki na wenyeji wa Shekemu, nao wenyeji wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa hila.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Mungu akaruhusu roho mbaya kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu, nao watu wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa hila.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 9:23
15 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa BWANA, ili alitimize neno lake, BWANA alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.


Basi mfalme hakuwasikia watu wale; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.


Yeye BWANA ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huku na huko akitapika.


Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.


Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.


Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.


Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;


lakini ikiwa basi moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki.


Basi Abimeleki alitawala juu ya Israeli kwa muda wa miaka mitatu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo