Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 9:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayumbayumbe juu ya miti?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini mzabibu ukajibu, ‘Mnadhani naweza kuacha shughuli yangu ya kuzalisha divai ambayo hufurahisha miungu na wanadamu, niende kujisumbua kuitawala miti?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini mzabibu ukajibu, ‘Mnadhani naweza kuacha shughuli yangu ya kuzalisha divai ambayo hufurahisha miungu na wanadamu, niende kujisumbua kuitawala miti?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini mzabibu ukajibu, ‘Mnadhani naweza kuacha shughuli yangu ya kuzalisha divai ambayo hufurahisha miungu na wanadamu, niende kujisumbua kuitawala miti?’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikatawale miti?’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikawe juu ya miti?’

Tazama sura Nakili




Waamuzi 9:13
9 Marejeleo ya Msalaba  

Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.


Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.


Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.


Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ungali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao.


Tena utasongeza nusu ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji, kwa sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.


na divai kwa sadaka ya kinywaji, robo ya hini, utaiandaa pamoja na sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa ajili ya kila mwana-kondoo.


na kwa sadaka ya kinywaji utasongeza sehemu ya tatu ya hini ya divai, kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu.


Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo