Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 8:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Ndipo hapo Zeba na Salmuna wakasema, Simama wewe utuue sisi; kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Basi Gideoni akasimama, akawaua Zeba na Salmuna, akazitwaa koja zilizokuwa katika shingo za ngamia wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Hapo Zeba na Salmuna wakasema, “Tuue wewe mwenyewe, maana hii ni kazi ya mtu mzima.” Gideoni akawaua yeye mwenyewe na kuchukua mapambo yao yaliyokuwa shingoni mwa ngamia wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Hapo Zeba na Salmuna wakasema, “Tuue wewe mwenyewe, maana hii ni kazi ya mtu mzima.” Gideoni akawaua yeye mwenyewe na kuchukua mapambo yao yaliyokuwa shingoni mwa ngamia wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Hapo Zeba na Salmuna wakasema, “Tuue wewe mwenyewe, maana hii ni kazi ya mtu mzima.” Gideoni akawaua yeye mwenyewe na kuchukua mapambo yao yaliyokuwa shingoni mwa ngamia wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Zeba na Salmuna wakasema, “Njoo ufanye hivyo wewe mwenyewe. ‘Alivyo mwanaume, ndivyo zilivyo nguvu zake.’ ” Hivyo, Gideoni akajitokeza na kuwaua, naye akayaondoa mapambo kwenye shingo za ngamia wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Zeba na Salmuna wakasema, “Njoo ufanye hivyo wewe mwenyewe. ‘Alivyo mtu, ndivyo zilivyo nguvu zake.’ ” Hivyo Gideoni akatoka mbele na kuwaua, naye akayaondoa mapambo kwenye shingo za ngamia zao.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 8:21
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ee Mungu, usistarehe, Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.


Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, Na wakuu wao wote kama Zeba na Zalmuna.


Ambao Walisema, Na tutamalaki makao ya Mungu.


Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;


Baadaye Yoshua akawapiga, na kuwaua, akawatundika katika miti mitano; nao wakawa wametundikwa katika hiyo miti hadi jioni.


Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.


Wakamwambia, Tumeshuka ili kukufunga, tupate kukutia katika mikono ya Wafilisti. Samsoni akawaambia, Niapieni ya kwamba ninyi wenyewe hamtaniua.


Kisha akamwambia Yetheri mwanawe mzaliwa wa kwanza, Haya, simama, uwaue hawa. Lakini huyo kijana hakutoa upanga wake; maana, akaogopa, kwa sababu alikuwa ni kijana tu.


Ndipo watu wa Israeli wakamwambia Gideoni, Tawala wewe juu yetu, wewe, na mwanao, na mjukuu wako pia; kwa kuwa wewe umetuokoa na mikono ya Midiani.


Na uzani wa hizo herini za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia wao.


Ndipo akamwita kwa haraka huyo kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, na kumwambia, Futa upanga wako, uniue, ili watu wasiseme juu yangu, Aliuawa na mwanamke. Basi huyo kijana wake akamchoma upanga, naye akafa.


Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde.


Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo