Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 8:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Basi akawatwaa hao wazee wa mji, na miiba ya nyikani na michongoma, akawafunza hao watu wa Sukothi kwayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Basi, akawachukua wazee wa Sukothi na kuwapa funzo wanaume wote kwa kuichana miili yao kwa miiba na mbigili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Basi, akawachukua wazee wa Sukothi na kuwapa funzo wanaume wote kwa kuichana miili yao kwa miiba na mbigili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Basi, akawachukua wazee wa Sukothi na kuwapa funzo wanaume wote kwa kuichana miili yao kwa miiba na mbigili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Akawachukua hao wazee wa mji, na kuwaadhibu wanaume wa Sukothi kwa kuwachapa kwa miiba na michongoma ya nyikani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Akawachukua hao viongozi wa mji na kuwafundisha watu wa Sukothi somo kwa kuwaadhibu kwa miiba na michongoma ya nyikani.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 8:16
7 Marejeleo ya Msalaba  

Wazawa wa Pahath-Moabu, wazawa wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili.


Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu.


Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu.


Mtu aliye mwema miongoni mwao ni kama mbigili; mtu aliye mwenye adili miongoni mwao ni mbaya kuliko boma la michongoma; hiyo siku ya walinzi wako, yaani, siku ya kujiliwa kwako, imefika; sasa kutatokea kufadhaika kwao.


Kisha akaufikia wale watu wa Sukothi, akawaambia, Tazama, Zeba na Salmuna, ambao ninyi mlinisimanga kwa ajili yao, mliposema, Je! Mikono ya Zeba na Salmuna iko sasa mikononi mwako wewe, hata tuwape watu wako waliochoka mikate?


Kisha akaubomoa mnara wa Penieli, na kuwaua watu wa mji huo.


Ndipo Gideoni akasema, Kwa sababu hii, hapo BWANA atakapokuwa amewatia Zeba na Salmuna mkononi mwangu, ndipo nitaipura miili yenu kwa miiba ya nyikani, na kwa michongoma.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo