Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 6:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Usiku huo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Gideoni, “Chukua fahali mmoja wa baba yako, fahali yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako na kuvunja sanamu ya Ashera iliyo karibu nayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Usiku huo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Gideoni, “Chukua fahali mmoja wa baba yako, fahali yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako na kuvunja sanamu ya Ashera iliyo karibu nayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Usiku huo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Gideoni, “Chukua fahali mmoja wa baba yako, fahali yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako na kuvunja sanamu ya Ashera iliyo karibu nayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Usiku ule ule Mwenyezi Mungu akamwambia, “Mchukue ng’ombe dume wa baba yako, yule wa pili mwenye miaka saba, ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate nguzo ya Ashera iliyo karibu nayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Usiku ule ule bwana akamwambia, “Mchukue ng’ombe dume wa baba yako, yaani, yule wa pili mwenye miaka saba, na ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate Ashera iliyo karibu nayo.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 6:25
14 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu.


Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.


Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako.


Nitakuwa na mwenendo usio na hatia; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu.


Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunjavunja nguzo zao, na kuyakatakata maashera yao.


Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.


Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.


Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;


Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.


Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomoeni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.


Wana wa Israeli walifanya mambo maovu mbele za macho ya BWANA, na wakawatumikia Mabaali.


Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, nao wakamsahau BWANA, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi.


ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo