Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 5:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Kutoka Efraimu waliteremka wao ambao shina lao ni katika Amaleki, Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako. Kutoka Makiri walishuka makamanda, Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kutoka Efraimu waliteremka bondeni, wakafuata ndugu zao watu wa Benyamini; kutoka Makiri walishuka makamanda, kutoka Zebuluni maofisa wakuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Kutoka Efraimu waliteremka bondeni, wakafuata ndugu zao watu wa Benyamini; kutoka Makiri walishuka makamanda, kutoka Zebuluni maofisa wakuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kutoka Efraimu waliteremka bondeni, wakafuata ndugu zao watu wa Benyamini; kutoka Makiri walishuka makamanda, kutoka Zebuluni maofisa wakuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Baadhi yao walitoka Efraimu, ambao chimbuko lao ni Amaleki; Benyamini alikuwa miongoni mwa watu waliokufuata. Kutoka Makiri wakashuka viongozi, na kutoka Zabuloni wale washikao fimbo ya jemadari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki; Benyamini akiwa miongoni mwa watu waliokufuata. Kutoka Makiri wakashuka viongozi, na kutoka Zabuloni wale washikao fimbo ya jemadari.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 5:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.


Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.


Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini.


Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali.


Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!


Huyo Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, akazikwa huko Pirathoni katika nchi ya Efraimu, katika nchi ya vilima ya Waamaleki.


Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende.


Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia.


Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.


Debora akamwambia Baraka, Haya! Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo BWANA amemtia Sisera katika mkono wako. Je! BWANA hakutoka atangulie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabori, na watu elfu kumi wakamfuata.


Ndipo waliteremka mabaki ya waungwana na ya watu; BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo