Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 5:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji, Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA; Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli. Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Imbeni kupita wanamuziki kwenye visima vya maji, tangazeni ushindi wa Mwenyezi-Mungu, ushindi kwa wakulima wake katika Israeli. Ndipo watu wa Mwenyezi-Mungu waliposhuka malangoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Imbeni kupita wanamuziki kwenye visima vya maji, tangazeni ushindi wa Mwenyezi-Mungu, ushindi kwa wakulima wake katika Israeli. Ndipo watu wa Mwenyezi-Mungu waliposhuka malangoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Imbeni kupita wanamuziki kwenye visima vya maji, tangazeni ushindi wa Mwenyezi-Mungu, ushindi kwa wakulima wake katika Israeli. Ndipo watu wa Mwenyezi-Mungu waliposhuka malangoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 kuhusu sauti za waimbaji mahali pa kunyweshea maji. Wanasimulia matendo ya haki ya Mwenyezi Mungu, matendo ya haki ya mashujaa wake katika Israeli. “Ndipo watu wa Mwenyezi Mungu walipoteremka malangoni pa mji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 juu ya sauti za waimbaji mahali pa kunyweshea maji. Wanasimulia matendo ya haki ya bwana, matendo ya haki ya mashujaa wake katika Israeli. “Ndipo watu wa bwana walipoteremka malangoni pa mji.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 5:11
19 Marejeleo ya Msalaba  

Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji wakati wa jioni, wakati ambapo wanawake wanakwenda kuteka maji.


Naye akaangalia, na tazama, kiko kisima kondeni, na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu nacho, kwa sababu katika kisima kile hunywesha makundi; na palikuwa na jiwe kubwa juu ya kinywa cha kisima.


Makundi yote hukusanyika huko, watu wakabingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake.


Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,


Watasimulia juu ya ukuu wa wema wako mwingi. Na wataiimba haki yako kwa sauti.


Lakini mimi nitakutumainia daima Na nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.


Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.


Naye atakuwa roho ya hukumu ya haki kwake yeye aketiye ili ahukumu; naye atakuwa nguvu kwao walindao langoni.


Simama langoni pa nyumba ya BWANA, ukatangaze hapo neno hili, ukisema, Sikilizeni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaoingia katika malango haya ili kumwabudu BWANA.


Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa.


Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani.


Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni yaliyotukia toka Shitimu hadi Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.


watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga ukelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.


Akajichagulia sehemu ya kwanza, Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria; Akaja pamoja na wakuu wa watu, Akaitekeleza haki ya BWANA, Na hukumu zake kwa Israeli.


kwamba binti za Israeli waende mwaka baada ya mwaka ili kumkumbuka huyo mwana wa Yeftha, Mgileadi, siku nne katika mwaka.


Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arubaini wa Israeli?


Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo