Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 4:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Yaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, “Bwana wangu, karibu kwangu, wala usiogope.” Akaingia hemani mwake, akamfunika kwa blanketi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Yaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, “Bwana wangu, karibu kwangu, wala usiogope.” Akaingia hemani mwake, akamfunika kwa blanketi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Yaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, “Bwana wangu, karibu kwangu, wala usiogope.” Akaingia hemani mwake, akamfunika kwa blanketi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Yaeli akaenda kumlaki Sisera na kumwambia, “Karibu, bwana wangu, karibu ingia ndani kabisa. Usiogope.” Basi Sisera akaingia ndani ya hema la Yaeli, naye akamfunika kwa blanketi nene.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Yaeli akaenda kumlaki Sisera na kumwambia, “Karibu, bwana wangu, karibu ingia ndani kabisa. Usiogope.” Basi Sisera akaingia ndani ya hema ya Yaeli, naye akamfunika kwa blanketi nene.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 4:18
3 Marejeleo ya Msalaba  

Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria.


Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.


Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo