Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 21:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Wana wa Israeli wakasema, Katika hizi kabila zote za Israeli ni ipi isiyofika katika mkutano kumkaribia BWANA? Kwa maana walikuwa wameweka kiapo kikuu kuhusu huyo asiyefika kumkaribia BWANA huko Mispa, huku wakisema, Hakika yake atauawa huyo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kisha wakaulizana, “Je, miongoni mwa makabila yote ya Israeli kuna kikundi chochote ambacho hakikuhudhuria mkutano uliofanyika mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Walikuwa wamefanya kiapo kwamba mtu yeyote ambaye hatahudhuria mbele ya Mwenyezi-Mungu huko Mizpa ni lazima auawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kisha wakaulizana, “Je, miongoni mwa makabila yote ya Israeli kuna kikundi chochote ambacho hakikuhudhuria mkutano uliofanyika mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Walikuwa wamefanya kiapo kwamba mtu yeyote ambaye hatahudhuria mbele ya Mwenyezi-Mungu huko Mizpa ni lazima auawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ndipo Waisraeli wakauliza, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikukusanyika mbele za Mwenyezi Mungu?” Kwa kuwa walikuwa wameapa kiapo kikuu kuwa yeyote asiyefika mbele za Mwenyezi Mungu huko Mispa, kwa hakika angeuawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ndipo Waisraeli wakasema, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikufika katika mkutano kumkaribia bwana?” Kwa kuwa walikuwa wameweka kiapo kikuu kuwa yeyote asiyefika mbele za bwana huko Mispa, kwa hakika angeuawa.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 21:5
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.

Basi watu wa Israeli walikuwa wameapa huko katika Mispa, wakisema, Hapana mtu yeyote kwetu sisi atakayemwoza binti yake kumpa Benyamini.

Lakini sisi hatuwezi kuwaoza binti zetu kwa maana wana wa Israeli walikuwa wameapa, wakisema, Na alaaniwe huyo atakayempa Benyamini mke.

Nao wana wa Israeli wakahuzunika kwa ajili ya ndugu yao Benyamini, wakasema, Kabila moja imekatiliwa mbali na Israeli hivi leo.

Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA, Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.

Akachukua fahali wawili waliofungwa nira, akawakatakata vipande, kisha akawatuma wajumbe kuvipeleka vile vipande kote katika Israeli, wakisema, Yeyote ambaye hatamfuata Sauli na Samweli, ng'ombe wake watafanyiwa vivi hivi. Basi utisho wa BWANA ukawaangukia wale watu, wakatoka kwa pamoja.

Nao watu wa Israeli walisumbuka sana siku ile; lakini Sauli alikuwa amewaapisha watu, akisema, Na alaaniwe mtu awaye yote alaye chakula chochote hadi jioni, nipate kujilipiza kisasi juu ya adui zangu. Basi hakuna mtu miongoni mwao aliyeonja chakula.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo