Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 21:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 kaeni macho; kisha tazameni, kisha hao binti za Shilo watakapotoka ili wacheze katika hiyo michezo, basi tokeni mizabibuni, na kila mtu na ajishikie mke katika hao binti za Shilo, kisha mrudi katika nchi ya Benyamini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Muwe macho. Wasichana wa Shilo watakapotoka nje kucheza wakati wa sikukuu, tokeni kwenye mizabibu na kila mtu ajinyakulie msichana mmoja awe mkewe. Kisha mrudi katika nchi ya Benyamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Muwe macho. Wasichana wa Shilo watakapotoka nje kucheza wakati wa sikukuu, tokeni kwenye mizabibu na kila mtu ajinyakulie msichana mmoja awe mkewe. Kisha mrudi katika nchi ya Benyamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Muwe macho. Wasichana wa Shilo watakapotoka nje kucheza wakati wa sikukuu, tokeni kwenye mizabibu na kila mtu ajinyakulie msichana mmoja awe mkewe. Kisha mrudi katika nchi ya Benyamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 na mkae macho. Wasichana wa Shilo watakapojiunga kwenye kucheza, tokeni kwenye hayo mashamba ya mizabibu, na kila mmoja ajinyakulie mke kutoka miongoni mwa hao wasichana wa Shilo, nanyi mwende nao katika nchi ya Benyamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 nanyi mwangalie. Wasichana wa Shilo watakapojiunga kwenye kucheza, ninyi tokeni kwenye hayo mashamba ya mizabibu na kila mmoja akamate mwanamke mmoja toka miongoni mwa hao wasichana wa Shilo na mwende nao katika nchi ya Benyamini.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 21:21
13 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.


Daudi akamwambia Mikali, Ilikuwa mbele za BWANA, aliyenichagua mimi juu ya baba yako, na juu ya nyumba yake, ili kuniweka niwe mkuu juu ya watu wa BWANA, juu ya Israeli; kwa hiyo mimi nitacheza mbele za BWANA.


Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.


Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;


Na Miriamu, nabii mwanamke, dada yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.


Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;


Rudi, rudi, Mshulami, Rudi, rudi, ili sisi tukutazame. Kwani mnataka kumtazama Mshulami, Kama kutazama ngoma ya Mahanaimu?


Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao.


Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;


Lakini kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki.


Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na akichezacheza; naye alikuwa ni mwanawe wa pekee; hakuwa na mwingine, wa kiume wala binti.


Basi wakawaagiza hao wana wa Benyamini wakisema, Haya, endeni, mkaotee katika mashamba ya mizabibu,


Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo