Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 21:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Basi Benyamini wakarudi wakati huo; kisha wakawapa wale wanawake waliowasalimisha katika hao wanawake wa Yabesh-gileadi; lakini wanawake hao hawakuwatosha.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Wanaume hao wa kabila la Benyamini wakawarudia hao wenzao wakati huohuo. Basi wakapewa wale wanawake ambao walikuwa wamesalimishwa huko Yabesh-gileadi. Lakini wanawake hao hawakuwatosha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Wanaume hao wa kabila la Benyamini wakawarudia hao wenzao wakati huohuo. Basi wakapewa wale wanawake ambao walikuwa wamesalimishwa huko Yabesh-gileadi. Lakini wanawake hao hawakuwatosha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Wanaume hao wa kabila la Benyamini wakawarudia hao wenzao wakati huohuo. Basi wakapewa wale wanawake ambao walikuwa wamesalimishwa huko Yabesh-gileadi. Lakini wanawake hao hawakuwatosha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Basi Wabenyamini wakarudi wakati ule, nao wakapewa wale wanawali wa Yabesh-Gileadi waliohifadhiwa. Lakini hawakuwatosha wanaume wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Basi Wabenyamini wakarudi nyumbani mwao, wakapewa wale wanawali wa Yabeshi-Gileadi waliowaponya. Lakini hawakuwatosha wanaume wote.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 21:14
7 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

Lakini wanaume mia sita wakageuka, wakakimbilia upande wa nyikani hadi katika jabali la Rimoni, wakakaa kwenye hilo jabali la Rimoni muda wa miezi minne.

Nao wakapata katika wenyeji wa Yabesh-gileadi wanawali mia nne, ambao hawajamjua mwanamume kwa kulala naye; basi wakawaleta kambini huko Shilo, ulioko katika nchi ya Kanaani.

Basi mkutano ukatuma watu na kunena na wana wa Benyamini waliokuwako huko katika jabali la Rimoni, wakawatangazia amani.

Nao watu wakawahurumia Wabenyamini, kwa sababu BWANA alikuwa amefanya pengo katika hayo makabila ya Israeli.

Kisha baba zao au ndugu zao watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa hisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; na kwa kuwa hamkuwapa wao, la sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia.

Basi wakasema, Ni ipi katika makabila ya Israeli ambayo haikufika mbele ya Bwana huko Mispa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo