Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 20:48 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

48 Kisha watu wa Israeli wakageuka tena kuwaendea wana wa Benyamini, wakawapiga kwa makali ya upanga, huo mji mzima, na hao wanyama wa mji, na kila kitu walichokiona; tena miji yote waliyoiona wakaiteketeza kwa moto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 Waisraeli wakawageukia watu wengine wa kabila la Benyamini, wakawaua wote: Wanaume, wanawake, watoto na wanyama. Na miji yote waliyoikuta huko wakaiteketeza moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 Waisraeli wakawageukia watu wengine wa kabila la Benyamini, wakawaua wote: Wanaume, wanawake, watoto na wanyama. Na miji yote waliyoikuta huko wakaiteketeza moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 Waisraeli wakawageukia watu wengine wa kabila la Benyamini, wakawaua wote: wanaume, wanawake, watoto na wanyama. Na miji yote waliyoikuta huko wakaiteketeza moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 Waisraeli wakarudi na kuwaua kwa upanga Wabenyamini wote, pamoja na wanyama na kila walichokipata. Pia kila mji waliouona wakauchoma kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

48 Waisraeli wakarudi na kuua watu wote wa Benyamini, pamoja na wanyama na kila walichokikuta. Pia kila mji waliouona waliuchoma moto.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 20:48
7 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wanajeshi, aliowarudisha Amazia, wasiende naye vitani, hao wakaiteka miji ya Yuda, tangu Samaria mpaka Beth-horoni, wakawapiga watu elfu tatu, wakachukua nyara nyingi.


Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.


Lakini wanaume mia sita wakageuka, wakakimbilia upande wa nyikani hadi katika jabali la Rimoni, wakakaa kwenye hilo jabali la Rimoni muda wa miezi minne.


Basi watu wa Israeli walikuwa wameapa huko katika Mispa, wakisema, Hapana mtu yeyote kwetu sisi atakayemwoza binti yake kumpa Benyamini.


Wana wa Benyamini wakafanya hivyo, wakajitwalia wake, kulingana na hesabu yao, katika hao waliocheza, wakawachukua wakaenda nao; kisha wakaenda kuurudia urithi wao, na kuijenga miji na kuishi humo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo