Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 20:46 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

46 Basi jumla ya watu wa Benyamini waliouawa siku ile walikuwa ni watu elfu ishirini na tano waliokuwa wapiganaji vita; wote hao walikuwa ni mashujaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Jumla ya watu wote wa kabila la Benyamini waliouawa siku hiyo ilikuwa 25,000, askari hodari wa kutumia silaha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Jumla ya watu wote wa kabila la Benyamini waliouawa siku hiyo ilikuwa 25,000, askari hodari wa kutumia silaha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Jumla ya watu wote wa kabila la Benyamini waliouawa siku hiyo ilikuwa 25,000, askari hodari wa kutumia silaha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Siku hiyo wakawaua Wabenyamini elfu ishirini na tano wenye panga, wapiganaji hodari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Siku ile wakawaua Wabenyamini 25,000 waliokuwa mashujaa wa vita.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 20:46
5 Marejeleo ya Msalaba  

Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, wanaume elfu ishirini na sita waliokuwa na silaha, mbali na hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.


BWANA akampiga Benyamini mbele ya Israeli; na wana wa Israeli waliangamiza wanaume elfu ishirini na tano na mia moja, wa Benyamini siku hiyo; wote hao waliokuwa wenye kutumia upanga.


Kisha wakageuka na kukimbilia upande wa nyika hadi katika jabali la Rimoni; nao wakaokota katika watu hao katika njia kuu wanaume elfu tano; wakawaandamia kwa kasi mpaka Gidomu, nako wakawaua wengine wao watu elfu mbili.


Lakini wanaume mia sita wakageuka, wakakimbilia upande wa nyikani hadi katika jabali la Rimoni, wakakaa kwenye hilo jabali la Rimoni muda wa miezi minne.


Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila la Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo