Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 20:41 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

41 Ndipo watu wa Israeli wakageuka, na watu wa Benyamini walishtushwa; kwa kuwa waliona ya kwamba wamefikiwa na maafa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Ndipo Waisraeli wakageuka, na watu wa kabila la Benyamini wakakumbwa na fadhaa kwani sasa waliona kuwa kuangamia kwao kulikuwa kumekaribia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Ndipo Waisraeli wakageuka, na watu wa kabila la Benyamini wakakumbwa na fadhaa kwani sasa waliona kuwa kuangamia kwao kulikuwa kumekaribia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Ndipo Waisraeli wakageuka, na watu wa kabila la Benyamini wakakumbwa na fadhaa kwani sasa waliona kuwa kuangamia kwao kulikuwa kumekaribia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Ndipo Waisraeli wakawageukia, nao Wabenyamini wakatiwa hofu, kwa kuwa walitambua kwamba maafa yamewajia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Ndipo watu wa Israeli wakawageukia, nao Wabenyamini wakatiwa hofu, kwa kuwa walitambua kwamba maafa yamewajia.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 20:41
14 Marejeleo ya Msalaba  

Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.


Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.


Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi.


Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.


Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?


watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.


Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.


Kisha hapo hao watu wa Ai walipotazama nyuma yao, wakaona, na tazama, moshi wa huo mji ulikuwa unapaa juu kwenda mawinguni, nao hawakuwa na nguvu za kukimbia huku wala huku; na wale watu waliokuwa wamekimbia kwenda nyikani wakageuka na kuwarudia hao waliokuwa wakiwafuatia.


Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo