Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 20:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Wana wa Benyamini wakasema, Wamepigwa mbele yetu kama wali. Lakini wana wa Israeli wakasema, Haya, na tukimbie, na kuwavuta wauache mji waende katika njia kuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Watu wa Benyamini wakafikiri, “Tumewapiga kama nyakati zilizopita.” Lakini Waisraeli wakasema, “Sisi tukimbie ili tuwavute mbali na mji hadi kwenye njia kuu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Watu wa Benyamini wakafikiri, “Tumewapiga kama nyakati zilizopita.” Lakini Waisraeli wakasema, “Sisi tukimbie ili tuwavute mbali na mji hadi kwenye njia kuu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Watu wa Benyamini wakafikiri, “Tumewapiga kama nyakati zilizopita.” Lakini Waisraeli wakasema, “Sisi tukimbie ili tuwavute mbali na mji hadi kwenye njia kuu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Wabenyamini walipokuwa wakiambiana, “Wanapigwa mbele yetu kama hapo awali,” nao Waisraeli waliambiana, “Turudini nyuma ili tuwavute wauache mji, waende kuelekea barabarani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Wabenyamini wakafikiri, “Wanapigwa mbele yetu kama hapo kwanza.” Waisraeli wakasema, “Sisi na turudi nyuma ili tuwavute wauache mji waende kuelekea barabarani.”

Tazama sura Nakili




Waamuzi 20:32
6 Marejeleo ya Msalaba  

na mimi, na watu wote walio pamoja nami, tutaukaribia mji; kisha itakuwa, hapo watakapotoka nje kupigana nasi, kama walivyofanya hapo kwanza, sisi tutakimbia mbele yao;


nao watatoka nje watufuate, hadi tuwavute waende mbali na mji wao; kwa kuwa watasema, Wakimbia mbele yetu, kama walivyofanya kwanza; nasi tutakimbia mbele yao;


Nao wana wa Benyamini wakatoka waende kupigana nao, wakavutwa waende mbali na huo mji; kisha wakaanza kuwapiga na kuwaua Waisraeli wapatao thelathini, kama walivyofanya hapo awali, kwa kuwaua katika hizo njia kuu, zielekeazo Betheli, na Gibea, na katika nchi tambarare.


Basi hao watu wote wa Israeli wakaondoka mahali pao wakajipanga huko Baal-tamari; na hao wenye kuvizia wa Israeli wakatoka mahali hapo walipokuwa, hata Maare-geba.


Nao watu wa Israeli walipogeuka katika ile vita, Benyamini naye akaanza kupiga na kuwaua watu wa Israeli kama watu thelathini; kwani walisema, Hakika yetu wamepigwa mbele yetu, vile vile kama katika ile vita ya kwanza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo