Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 20:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea siku ya pili, wakawaua watu elfu kumi na nane tena katika watu wa Israeli; hao wote walikuwa wamejihami.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Siku hiyo ya pili watu wa kabila la Benyamini walitoka Gibea na kuwashambulia Waisraeli, wakawaangusha chini Waisraeli 18,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Siku hiyo ya pili watu wa kabila la Benyamini walitoka Gibea na kuwashambulia Waisraeli, wakawaangusha chini Waisraeli 18,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Siku hiyo ya pili watu wa kabila la Benyamini walitoka Gibea na kuwashambulia Waisraeli, wakawaangusha chini Waisraeli 18,000.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Wakati huu, Wabenyamini walipotoka Gibea ili kupigana na Waisraeli, wakawaua wanaume elfu kumi na nane wenye panga.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Wakati huu, Wabenyamini walipotoka Gibea ili kupigana nao, wakawaua watu Waisraeli 18,000, wote wakiwa wamejifunga panga.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 20:25
11 Marejeleo ya Msalaba  

La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?


Benyamini ni mbwamwitu mwenye kuraruararua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.


Mawingu na giza vyamzunguka, Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.


Ee Israeli, umefanya dhambi tangu siku za Gibea; huko ndiko walikosimama; Je, vita juu ya wana wa uovu hakitawapata katika Gibea?


Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!


Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,


Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)


Wana wa Benyamini wakatoka Gibea, wakawaua watu elfu ishirini na mbili katika Israeli siku hiyo.


Basi wana wa Israeli wakakaribia juu ya wana wa Benyamini siku ya pili.


Ndipo wana wa Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za BWANA, wakafunga siku hiyo hadi jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo