Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 20:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Lakini watu hao, watu wa Israeli, walijitia nguvu, wakaviandaa vile vita mara ya pili mahali pale walipojiandaa siku ya kwanza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Lakini Waisraeli wakajipa moyo, wakajipanga tena kwa vita mahali pale walipojipanga kwa mara ya kwanza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Lakini Waisraeli wakajipa moyo, wakajipanga tena kwa vita mahali pale walipojipanga kwa mara ya kwanza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Lakini Waisraeli wakajipa moyo, wakajipanga tena kwa vita mahali pale walipojipanga kwa mara ya kwanza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Lakini Waisraeli wakatiana moyo kila mmoja na mwenzake, nao wakachukua tena nafasi zao katika vile vita mahali pale walipokuwa siku ya kwanza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Lakini Waisraeli wakatiana moyo kila mmoja na mwenzake, nao wakajiweka kwenye nafasi zao katika vile vita mara ya pili mahali pale walipokuwa wamejiweka mara ya kwanza.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 20:22
7 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akamwambia yule mjumbe, Basi, mwambie Yoabu maneno haya, Jambo hili lisiwe baya machoni pako, maana upanga hula huyu kama unavyomla huyu; zidi kutia nguvu vita vyako juu ya mji ukauangushe; nawe mtie moyo.


Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Wakisema, Ni nani atakayeiona?


Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, wanaume elfu ishirini na sita waliokuwa na silaha, mbali na hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.


Nao watu wa Israeli, mbali na hao wa Benyamini, walihesabiwa kuwa ni wanaume elfu mia nne, wenye silaha; hao wote walikuwa ni watu wa vita.


Wana wa Benyamini wakatoka Gibea, wakawaua watu elfu ishirini na mbili katika Israeli siku hiyo.


Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za BWANA hadi jioni; wakamwuliza BWANA, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? BWANA akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye.


Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo